Nimeona mtaani watu wakiwa na maswali mengi juu ya kwanini Pi Coin haipo na haijalistiwa kwenye exchange ya Binance au masoko makubwa ya cryptocurrency kama Coinbase, Kraken, na KuCoin. Watu wengi wana matumaini makubwa juu ya Pi Network, lakini bado kuna changamoto kadhaa zinazokwamisha hii ishu. Hapa kwenye hii thread tunaenda kuchambua sababu kuu zinazoifanya Pi Coin kushindwa kulistiwa kwenye exchange ya Binance.
Point ya 1 ni kwamba Mainnet ya Pi network haijakamilika Kamilifu
Taarifa kutoka Pi Network zinaonesha bado Pi hawajafungua Open Mainnet kwa kila mtu. Kwa sasa, mtandao uko kwenye Enclosed Mainnet, ambapo miamala inaweza kufanyika tu kati ya watumiaji waliothibitishwa (KYC) ndani ya mfumo wa Pi Network. Bila blockchain kuwa wazi na kuruhusu miamala kwenye CEX (Centralized Exchanges), haiwezekani kwa Binance kulist Pi.
Point namba mbili ni kwamba Pi network wamekosa uwazi kuhusu teknolojia yao
Exchange kama Binance na masoko mengine makubwa huwa na viwango vya juu vya audition au ukaguzi wa kiufundi kabla ya kuorodhesha tokeni husika. Hadi sasa, Pi Network haijatoa whitepaper ya kina inayoelezea wazi vigezo vya blockchain yake, jinsi mining inavyofanya kazi, na mgawanyo wake wa sarafu kwa undani. Bila hizi taarifa, Binance imeona Pi Coin kama mradi usio na uhakika kwenye teknolojia.
Pia Pi network wameonekana kuwa na Changamoto za KYC (Know Your Customer)
Mojawapo ya kikwazo kikubwa kwa miners wa Pi ni mfumo wa KYC waliouweka ambao umekuwa ukihusisha kuchelewa kwa uthibitishaji wa akaunti. Binance haiwezi kuorodhesha sarafu yenye watumiaji wengi ambao bado hawajathibitishwa. Ili sarafu iwe na thamani kwenye soko, inapaswa kuwa na msingi thabiti wa watumiaji wanaoweza kufanya miamala huru.
Point nyingine ni kwamba Udhibiti na Sheria kwenye Pi network ni hafifu
Mpaka sasa soko la crypto linazidi kudhibitiwa na mamlaka za kifedha duniani. Binance inahakikisha kuwa sarafu zote zinazoingia kwenye soko lake zinakidhi vigezo vya kisheria na uwazi. Mpaka sasa, Pi Network haijatoa taarifa rasmi kuhusu jinsi inavyoshughulikia masuala ya compliance yaani kuzingatia sheria za kifedha, jambo linaloweza kuwafanya Binance kuwa waangalifu zaidi kabla ya kuorodhesha Pi.
Pi network pia Hawana Public Trading au uuzaji wa hadharani
Pi Coin bado haijaanza kuuzwa kwenye blockchain yoyote inayojulikana (kama Ethereum au Binance Smart Chain). Binance haiwezi kuorodhesha tokeni ambayo haiwezi kuuzwa kwa uwazi au kuhamishwa nje ya mfumo wake wa ndani. Mpaka Pi iweze kutumika kama sarafu huru, Binance haiwezi kuilist kwenye soko lake kwa ajili ya kufanyiwa miamala.
Sasa mtu anaweza akaniuliza swali kuwa
Je, Pi Coin Inaweza Kulistiwa Baadaye?
Jibu ni ndiyo, kuna uwezekano mkubwa. Hili litatokea ikiwa:
1.Mainnet itafunguliwa kwa kila mtu
2.Teknolojia itaweka mambo yake wazi zaidi
3.Watumiaji wengi watathibitisha akaunti zao kwa KYC
4.Pi itaruhusu open trading
5.Regulatory compliance itazingatiwa
Kwa sasa, ni vyema kuendelea kufuatilia maendeleo ya Pi Network na kuona hatua zitakazofuata.
Mwisho kabisa nakaribisha maoni yako ndugu msomaji!